Home > News> Taasisi ya JAMANI yatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya msingi kiwalani

Taasisi ya JAMANI yatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya msingi kiwalani

May 21, 2015

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), imepoke amchango wa madawati 50 kutoka Taasisi ya JAMANI (JAMANI Foundation) kwa ajili ya shule ya Msingi Kiwalani tarehe  18 Mei, 2015.

Msaada huu ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya ufadhili wa madawati 504 na vyoo kumi na mbili kuitoka Taasisi ya JAMANI (Jamani Foundation) kwa shule kumi na mbili za mkoa wa Dar es Salaam iliyotolewa tarehe 10. Machi. 2015. Thamani ya msaada huo ni  takribani shilingi milioni 65

Mnamo tarehe 10 Machi 2015, Taasisi hiyo ilitoa msaada wa madawati 104, na ahadi  ya madawati mengine 400 yaliyoahidiwa kutolewa  kwa awamu kadhaa ndani ya mwaka 2015, sambamba na ahadi ya  na  ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili  kwa shule nyinginezo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Msaada huo umewasilishwa na Meneja mkuu wa Jamani Foundation, ndugu Sadrudin Virji kwa niaba ya Jamani Fioundatiuon na Kupokelewa na Sylvia Lupembe ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji rasilimali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania  kwa nia ba ya Shule ya msingi Kiwalani.

Katika Uteuzi wa shule za kunufaika na msaada huu mkoani Dar es Salaam, Mamlaka ya Elimu Tanzania imezingatia mambo matatu, yaani; Ukubwa wa hitaji, ujirani kati ya shule na eneo analofanyia kazi mfadhili, na mapendekezo ya mfadhili na Mamlaka ya Elimu.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014, nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa madawati kwa asilimia arobaini na nne nukta nne (44.4%). Yaani katika kila watoto kumi wanaoenda shuleni, wastani wa watoto zaidi ya wanne hawakai katika madawati.  Aidha kwa Mkoa wa Dar es salaam pekee, unaupungufu ni madawati yapatayo 67 elfu (kwa shule za msingi).


Download

Share this: