Home > News> Taarifa kwa Umma Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Taarifa kwa Umma Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

June 22, 2016

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuadhimisha wiki ya UTUMISHI WA UMMA inawajulisha wananchi wote kuwa TAREHE 22 na 23 JUNI 2016, itatoa huduma maalum ya kupokea hoja, maoni, kero na malalamiko kuhusu huduma zetu.

Huduma hiyo itatolewa na Viongozi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania katika ofisi zetu zilizopo barabara ya kambarage kiwanja namba 771/3 mikocheni.

MUDAni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni. Pia tunapokea maoni kupitia tovuti yetu www.tea.or.tz, akaunti yetu ya facebook www.facebook.com/mamlakayaelimuau barua pepe info@tea.or.tz.

Karibu utoe MAONI, KERO, HOJA na MALALAMIKO ili tuweze kuboresha na kutoa huduma kwa ubora zaidi.

Tunaendelea kuwashukuru wadau wote wanaochangia Mfuko wa Elimu na tunaoendelea kushirikiana nao katika kutekeleza miradi mbalimbali yenye kusaidia kuongeza ubora na upatikanaji wa elimu nchini.

Wananchi na Wadau wote wa Elimu mnakaribishwa.

Imetolewa na;

KITENGO CHA MAWASILIANO NA MAHUSIANO

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA
Share this: