Home > Press Release> Mamlaka ya Elimu Tanzania kushirikisha makampuni kuchangia madawati

Mamlaka ya Elimu Tanzania kushirikisha makampuni kuchangia madawati

August 25, 2014

VIDOKEZO:

  • Mamlaka ya Elimu Tanzania kushirikisha makampuni kuchangia madawati

  • Madawati 2000 kutolewa kwa shule za msingi 12 za Dar es salaam

  • Wanafunzi zaidi ya 6000 kunufaika

  • Zaidi ya TZS 150,000,000 zatumika

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Mafuta TOTAL, benki ya KCB na shirika la Social Action Trust Fund imetoa ufadhili wa madawati 2000, yenye thamani ya shilingi milioni mia moja hamsini na sita (TZS 156,000,000) Kwa shule za msingi 1O za Mkoa wa Dar es salaam.

Shule zitakazonufaika na ufadhili huu ni chamazi, Mbande , Boko NHC, King’ong’ o, Hekima, Bwawani, Bunju , Goba , Kombo na Kingugi ambapo madawati haya yatatolewa mwezi septemba, 2014.

TEA kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta TOTAL na wadau wengine imeanzisha mpango huu wa miaka mitatu wa kufadhili wa madawati kwa shule zenye uhitaji mkubwa wa madawati na tumeanza na mkoa wa Dar es salaam. Aidha mpango huu ulianza mwaka 2013 kwa Total Kutoa madawati 1,000 na mwaka huu idadi imeongezeka kutokana na kuongezeka kwa wadau wanaochangia.

 Kutokana na tathmini ya mwaka 2013, Tanzania ina upungufu wa madawati 1,147,471. Uhitaji huu ni mkubwa hivyo basi tunakaribisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za umma, mashirika binafsi, asasi mbalimbali na watu binafsi kushiriki katika kupunguza changamoto hii.

Tunapenda kuutarifu umma kuwa, TEA imezingatia pia rai iliyotolewa na Waziri Mkuu ya kuhakikisha tatizo la madawati katika shule za mzingi linamalizika ifikapo mwezi Juni mwakani (2015) na hivyo kuipa kipaumbele .

Tunatoa pongezi kwa TOTAL, KBC na Social Action Trust Fund kwa kuonyesha njia na kwa niaba ya serikali na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tunatoa shukrani za dhati kwa makampuni haya.

 

_____________

Sylvia T. Lupembe

Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano

Mamlaka ya Elimu Tanzania

 +255 784 664433, +255 222775468/86, info@tea.or.tz,slupembe@tea.or.tz
Share this: