January 2021

ORODHA YA MAJINA YA WANUFAIKA WA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUENDELEZA UJUZI KWA MAKUNDI MAALUMU NA VIJANA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

1. Utangulizi

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mwaka 2017, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliipatia TEA jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazohusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi kwa lengo la kuzalisha ajira (ESPJ) unaotekelezwa na Wizara hiyo ukipata ufadhili toka Benki ya Dunia. Programu ya ESPJ ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Ujuzi (National Skills Development Strategy-NSDS: 2016-2021).

Maeneo muhimu yanayolengwa katika utekelezaji wa programu ya ESPJ ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji na pia kuongeza uwiano wa wataalam wa fani mbalimbali katika Sekta sita za kipaumbele (Kilimo na Kilimo Biashara, Utalii na huduma za Ukarimu, Nishati, Ujenzi, Uchukuzi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHEMA) zenye mchango mkubwa wa kiuchumi nchini.

Ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wenye mahitaji ya ujuzi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania imeanzisha Mpango wa Ufadhili (Bursary Scheme) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi. Mpango huu umelenga kuwezesha mafunzo ya ujuzi kwa vijana kutoka makundi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate uwezo wa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji zenye tija.

Tangazo la kukaribisha maombi ya ufadhili lilitangazwa mapema mwezi Septemba 2020 katika magazeti na tovuti ya TEA. Baada ya kupokea na kupitia maombi yaliyotumwa kuomba ufadhili, jumla ya wanufaika 2,102 wamekidhi vigezo vya kupatiwa Ufadhili wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi Kwa Makundi Maalumu na Vijana Wanaoishi Katika Mazingira Magumu. Orodha ya Wanufaika imeambatanishwa katika tangazo hili.

 

 

Orodha ya Majina ya wanufaika

English