June 2021

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) inapenda kuwatangazia wananchi wote kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara wa vifaa chakavu vilivyopo katika ofisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo Mikocheni B Mtaa wa Bima mkabala na kituo kidogo cha polisi cha Mikocheni. Mnada huo utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 28 mwezi Juni, 2021 saa nne (4.00) asubuhi.
Swahili