March 2023

TEA KWA KUSHIRIKIANA NA TAHA YANUFAISHA VIJANA KWENYE SEKTA YA KILIMO

Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 nchini Tanzania yalibainisha kuwa, asilimia 34.5 ya watanzania wote ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa. Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha vijana wanahusishwa kikamilifu katika miradi na programu za maendeleo kupitia mafunzo ya ujuzi na Ufundi stadi ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana katika ngazi zote.
English