MAKAMU WA RAIS, DKT. PHILLIP MPANGO APEWA MAELEZO KUHUSU UTEKELEZAJI WA MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (SDF)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango leo tarehe 12 Septemba 2022 ametembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  na kupewa maelezo kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na TEA kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia(WB).

 

TEA ni miongoni mwa za Taasisi zinazoshiriki maonyesho ya siku tatu ya  Mkutano  Mkuu wa 36 wa  Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania - ALAT yanayofanyika Jijini Mbeya kuanzia  tarehe 12 Septemba, 2022.

 

Mkurugenzi  Mkuu wa  TEA, Bahati Geuzye amesema mfuko wa SDF umetoa mafunzo kwa zaidi ya vijana elfu 37 kati ya  vijana elfu 38 wanaolengwa kupatiwa mafunzo hayo hadi ifikapo Desemba 2022.

 

Akijibu swali la Makamu wa Rais kuhusu idadi ya vijana wanaotoka kaya maskini walionufaika  na mafunzo ya kukuza ujuzi kupitia ufadhili wa SDF, Mkurugenzi Mkuu wa TEA alisema  zaidi ya vijana 1,627  wamepata mafunzo  hayo  hadi sasa na kwamba vijana zaidi kutoka kundi hilo watapatiwa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa lengo la kuwezesha kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.

 

Makamu wa Rais alikuwa mgeni ramsi katika mkutano mkuu wa 36 Jumuiya za  Tawala za Mitaa unaofanyika jijini  Mbeya kwa siku tatu