Mamlaka Ya Elimu Tanzania (Tea), Yatoa Ufadhili Wa Milioni 300 Kwa Chuo Kikuu Cha Sayansi Na Teknolojia Cha Mwalimu Julius K.Nyerere

Error message

Deprecated function: The each() function is deprecated. This message will be suppressed on further calls in _menu_load_objects() (line 579 of /home/teaor/public_html/includes/menu.inc).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kupitia Mfuko wa Elimu. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage.

 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (wa pili kulia) wakitiliana saini makubaliano ya ufadhili wa Shilingi Millioni 300 utakaotolewa na TEA kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi na kutengeneza mtaala katika Kampasi ya Butiama ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere, hafla hiyo fupi ilifanyika leo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Msafiri Jackson na kulia ni Mkurugenzi Uratibu na Ufadhili Miradi wa TEA Bibi Anna Magalla.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage akitoa shukrani kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ufadhili wa Shilingi Millioni300 utakaotolewa na mamlaka hiyo kusaidia Ujenzi wa jengo la ofisi za utawala na wakufunzi pamoja  na ununuzi wa samani za ofisi hizo na utengenezaji wa mtaala kwa mwaka wa masomo 2016/17. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bw. Joel Laurent.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (kulia) wakikabidhiana hati za makubaliano ya ufadhili wa Shilingi Millioni 300 utakaotolewa na TEA kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi na kutengeneza mtaala katika Kampasi ya Butiama ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere kwenye hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Prof. Lesakit Mellay Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philip Mulugo akipokea zawadi ya kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakati alipotembelea ofisi za mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa TEA Bibi Sylvia Lupembe.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philip Mulugo (wa nne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakati alipotembelea ofisi za mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bw. Joel Laurent.

 Wakuu wa Idara mbalimbali za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifurahia jambo na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philip Mulugo (katikati) nje ya ofisi za mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bw. Joel Laurent.