TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

 

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

 

Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) inapenda kuwatangazia wananchi wote kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara wa vifaa chakavu vilivyopo katika ofisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo Mikocheni B Mtaa wa Bima mkabala na kituo kidogo cha polisi cha Mikocheni.  Mnada huo utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 28 mwezi Juni, 2021 saa nne (4.00) asubuhi.

Vifaa vitakavyouzwa ni pamoja na gari moja aina ya Nissan Patrol, Kompyuta za mezani (Desktop), Kompyuta mpakato (Laptop) na vifaa vingine vya ofisini.

MASHARTI YA MNADA:

 

1.    Chombo/kifaa kitauzwa kama kilivyo mahali kilipo;

2.    Mnunuzi atalazimika kulipa amana papo hapo si chini ya asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya chombo/kifaa alichonunua, na kukamilisha malipo yote katika muda wa siku kumi na nne (14), kuanzia tarehe ya kifaa kunadiwa.  Kushindwa kufanya hivyo kutamuondolea mnunuzi haki zote za ununuzi wa chombo/kifaa kinachohusika na AMANA (Deposit) haitarudishwa;

3.    Mnunuzi atatakiwa kuondoa/kuchukua chombo alichonunua katika muda wa siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo;

4.    Ruhusa ya kuangalia vyombo hivyo itatolewa tarehe 25 na 26 mwezi Juni, 2021 kuanzia saa nne (4.00) asubuhi hadi saa kumi (10.00) jioni;

5.    Mnada utaanza saa nne (4.00) asubuhi katika ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo:

 

Bima Road Kitalu Na. 711, Mikocheni B

S.L.P. 34578, DAR ES SALAAM.

Simu:  255 22 2781079/181.

 

         MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA