WATUMISHI TEA WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA.

WATUMISHI TEA WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA.
Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekumbusha kufanya kazi kwa
kujituma na bidii ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali na umma wa watanzania.
Kauli hii ameitoa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka Dkt. Erasmus Kipesha mara
baada ya kuwasili katika ofisi za TEA Jijini Dodoma na kuwa na kikao kifupi na
watumishi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi Meneja wa Huduma za Sheria wa TEA, Bi
Christina Meela, amempongeza Dkt. Kipesha kwa uteuzi na kumhakikishia kuwa
watumishi wako tayari kushirikiana nae ili kufanikisha majukumu ya Mamlaka lakini pia
kutekeleza malengo ya Serikali.
Dkt. Kipesha aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TEA na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 23 Septemba 2023.