Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Karibu

Ni furaha yangu kubwa kuwakaribisha kwenye tovuti rasmi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

TEA imepewa dhamana ya kusimamia Mfuko wa Elimu na kuratibu ufadhili wa elimu kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwezesha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa nchini Tanzania.

Kupitia uhamasishaji madhubuti wa rasilimali, ubia wa kimkakati na usimamizi makini wa fedha za Mfuko wa Elimu wa Taifa, TEA inaunga mkono mipango inayolenga kushughulikia vipaumbele muhimu katika sekta ya elimu. Utekelezaji wetu unajumuisha kufadhili  ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu, upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, ukuzaji wa ujuzi, pamoja na programu nyingine zinazochangia kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kujifunza na kukuza nguvu kazi yenye ujuzi na tija.

 

Tunatambua kuwa maendeleo endelevu ya sekta ya elimu yanahitaji ushirikiano imara kati ya taasisi za Serikali, washirika wa maendeleo, sekta binafsi, jamii na wadau wengine. Kwa hiyo, TEA inaendelea kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha kuwa rasilimali zinazokusanywa kupitia Mfuko wa Elimu zinatumika kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji ili kuleta matokeo makubwa zaidi.

Tovuti hii inalenga kuwapatia wadau wetu na umma kwa ujumla taarifa kwa wakati na zinazopatikana kwa urahisi kuhusu dhamana, programu, miradi, mafanikio, machapisho, fursa na huduma za TEA. Tunawahimiza kutembelea Tovuti hii na kuendelea kushirikiana nasi tunapoendeleza maendeleo ya elimu nchini Tanzania.

TEA itaendelea kuhimiza ubunifu, kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali ili kusaidia vipaumbele vya Serikali katika sekta ya elimu.

Kwa mara nyingine tena, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

“Changia Mfuko wa Elimu; Boresha Miundombinu ya Elimu”

 

Dkt. Erasmus F. Kipesha
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)