Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma

Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma

Kazi kuu ya Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma ni kujenga na kudumisha taswira chanya ya Mamlaka pamoja na kuwezesha mawasiliano yenye ufanisi na wadau wa ndani na nje ya Mamlaka.

Majukumu ya Kitengo yanajumuisha kuandaa na kutekeleza mikakati ya mawasiliano, kusimamia mahusiano na vyombo vya habari, kuhabarisha  umma, kuratibu mawasiliano ya ndani, pamoja na kusimamia mawasiliano wakati wa changamoto au migogoro.

Aidha, Kitengo huandaa na kusimamia maudhui ya mawasiliano, kuratibu matukio na shughuli za Mamlaka, pamoja na kufuatilia mtazamo wa umma kuhusu Mamlaka ili kuboresha mikakati ya mawasiliano na kuimarisha sifa na taswira ya TEA.