Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Majukumu Yetu

Majukumu Yetu

  • Kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha na endelevu kwa ajili ya Mfuko wa Elimu.
  • Kushauri Serikali kuhusu vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha na endelevu katika Mfuko.
  • Kukuza elimu na mafunzo kulingana na mahitaji, kwa kuzingatia mipango na sera za kitaifa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  • Kutumia fedha zilizowekwa kwenye Mfuko kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza elimu.
  • Kuandaa na kupitia mara kwa mara kanuni za ugawaji na utoaji wa fedha kwa ngazi mbalimbali za elimu.
  • Kufuatilia matumizi ya fedha zilizotolewa na kuhakikisha kuwa zinatumika kwa kuzingatia malengo ya Mfuko.
  • Kupokea zawadi, michango, ruzuku na fedha nyingine kwa niaba ya Mfuko.
  • Kuanzisha na kuendeleza uhusiano au ushirikiano na taasisi za ndani na za kimataifa.