Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Kurugenzi ya Utafutaji Rasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu

Kurugenzi ya Utafutaji Rasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu

Kurugenzi ya Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu, ina jukumu la kuhakikisha upatikanaji  endelevu wa rasilimali ( fedha na vifaa) kupitia ushirikiano wa kimkakati, uhamasishaji na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, kwa lengo la kusaidia maendeleo ya elimu nchini. Kurugenzi husimamia sera na taratibu za utoaji wa ruzuku/ ufadhili kwa ajili ya  miradi ya elimu kwa kuhakikisha kuwa rasilimali zinaelekezwa kwenye miradi inayokidhi mahitaji ya miundombinu ya elimu. Aidha, Kurugenzi hufanya tathmini ya miradi na kupima athari zake ili kuhakikisha matumizi yenye ufanisi ya fedha za Mfuko. Pia, hujenga na kuendeleza ushirikiano na wadau pamoja na wafadhili, na kusimamia utendaji ndani ya timu yake ili kufanikisha dhamira ya TEA ya kusaidia jitihada za serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu  bora kwa usawa nchini Tanzania.

Kurugenzi ina Sehemu mbili (2):

  1. Sehemu ya Usimamizi Miradi ya Elimu
  2. Sehemu ya Utafutaji Rasilimali na Hamasa