Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Bweni La Wasichana Kichema – Sumbawanga Kunufaisha...

Bweni La Wasichana Kichema – Sumbawanga Kunufaisha Wanafunzi 80

08 Oct, 2026
Bweni La Wasichana Kichema – Sumbawanga Kunufaisha Wanafunzi 80

Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kichema, Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa Region, limekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wanafunzi. Bweni hilo, lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80, limejengwa kwa fedha kutoka Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na TEA, ambapo kiasi cha shilingi milioni 120 kimetumika.

Ujenzi wa bweni hilo umeboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kujifunzia kwa kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kila siku. Hatua hiyo pia imeongeza usalama, muda wa kujisomea na kuimarisha ufaulu wa kitaaluma.

Meneja Miradi wa TEA, Mwafatuma Mohamed, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kusimamia vyema utekelezaji wa mradi huo na kuhakikisha bweni linakamilika na kuanza kutumika kama ilivyokusudiwa.