Elimu ya Amali inaendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo unaowawezesha kujiajiri na kujitegemea hata kabla ya kuhitimu elimu ya sekondari.
Katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga, Jijini Mbeya, Sadiki Reuben Mlimandoki, mwanafunzi wa Kidato cha Tatu anayesomea ufundi umeme, tayari ameanza kutumia ujuzi alioupata shuleni kufanya kazi za ufundi na kupata kipato.
“Wiki iliyopita nilipata kazi ya kufunga mfumo wa umeme katika nyumba mpya na nililipwa fedha,” anasema Sadiki, akieleza kuwa kipato hicho kinamsaidia kugharamia baadhi ya mahitaji yake.
Mwanafunzi mwingine, Frank Elias Hussen, anasema mafunzo hayo yamempa matumaini ya kutimiza ndoto yake ya kuwa fundi umeme, akibainisha kuwa mahitaji ya mafundi wenye ujuzi ni makubwa katika jamii.
Mafanikio hayo yamewezeshwa pia na uwekezaji wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Shule hiyo imepokea zaidi ya Shilingi milioni 276 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya mafunzo ya vitendo katika karakana za ufundi, umeme, ujenzi, kompyuta na uashi.
Kwa mujibu wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari wa mwaka 2023, Mkondo wa Elimu ya Amali unalenga kuwajengea wanafunzi ujuzi wa ufundi na ujasiriamali unaowawezesha kujiajiri, kuajiriwa na kuanzisha ajira kwa wengine.
Uzoefu wa wanafunzi wa Iyunga unaonesha kuwa uwekezaji katika Elimu ya Amali ni uwekezaji katika ujuzi, ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...