Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
TEA YATUNUKIWA KOMBE LA USHINDI WA MCHEZO WA KARAT...

TEA YATUNUKIWA KOMBE LA USHINDI WA MCHEZO WA KARATA

26 Nov, 2026
TEA YATUNUKIWA KOMBE LA USHINDI WA MCHEZO WA KARATA

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetunukiwa kombe la ushindi katika mchezo wa karata kwa wanawake, kufuatia mwakilishi wake, Bi. Usuil Israel, kuibuka mshindi katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) 2026, yaliyofikia kilele tarehe 20 Novemba 2026, Mkoani Morogoro.

Tuzo hiyo inatambua mafanikio ya TEA katika mchezo huo, ambapo mwakilishi wake alionesha umahiri na ushindani mkubwa, na kuipeperusha vyema bendera ya Mamlaka.

TEA ilishiriki kikamilifu katika mashindano hayo yaliyodumu kwa wiki mbili, ikishiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, riadha, kurusha mishale na mbio za baiskeli.

Katika mchezo wa kurusha mishale, mwakilishi mwingine wa TEA, Bi. Zawadi Manyama, aliibuka mshindi wa nafasi ya nne, huku Tito Mathayo akifanikiwa kumaliza mbio za baiskeli za kilometa 50.

Mafanikio hayo yanaonesha ari, mshikamano na uwezo wa watumishi wa TEA katika kushiriki na kufanya vizuri katika michezo mbalimbali.

Hongera TEA kwa ushindi na mafanikio haya!