Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imewasilisha mafanikio ya utekelezaji wa miradi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, ikionyesha jinsi taasisi hiyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika elimu nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Erasmus Kipesha, ametoa wasilisho hilo ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, kwa lengo la kuwawezesha kuelewa vizuri majukumu na utendaji wa TEA na taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Katika kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi kuhusu jinsi TEA inavyosimamia na kuendesha Mfuko wa Taifa wa Elimu, ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo ya shule, mabweni, maabara, na vyoo.
Dkt. Kipesha alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026 hadi wmaka 2025/2026, jumla ya miradi 1,711 yenye thamani ya Sh. bilioni 128.5 imetekelezwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Elimu, ikionyesha mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya elimu na kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto wa Kitanzania
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...