Ujenzi wa bweni maalum lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 katika Shule ya Msingi Mwenge, jijini Mbeya, umeongeza fursa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata mazingira bora ya kujifunzia na kuishi shuleni.
Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Aness Mwakaje, amesema bweni hilo, lililogharimu Shilingi milioni 142.9 na kujengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ni bweni la kwanza na pekee kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum jijini Mbeya.
Amesema bweni hilo limepunguza changamoto kwa wazazi ambao hapo awali walilazimika kuwasindikiza na kuwachukua watoto wao kila siku, hivyo kuwawezesha kushiriki zaidi katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu, Bw. Ally Abdallah, amesema katika miaka ya fedha 2021/2022 na 2022/2023, Halmashauri ya Jiji la Mbeya ilipokea ufadhili wa miradi mbalimbali kutoka TEA wenye thamani ya takribani Shilingi milioni 556, ikiwemo madarasa, vyoo na mabweni.
Ameongeza kuwa Halmashauri imetenga Shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujenga uzio wa bweni hilo, huku Serikali Kuu ikiendelea na ujenzi wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume wenye mahitaji maalum.
Wadau wa elimu katika Kata ya Luanda wameipongeza TEA kwa mradi huo, wakisema utawawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira salama na wezeshi zaidi, huku wakiahidi kushirikiana katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo.
Shule ya Sekondari Katoro iliyopo mkoani Geita imepokea zaidi ya Shilingi...
Shule ya Sekondari Chief Sarwatt iliyopo Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, imepok...
Jumla ya shule 167 za sekondari nchini zinatekeleza mtaala wa Elimu ya Amali una...
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), kwa kushirikiana na Mamlaka ya E...
Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), una...