Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
TEA Yajenga Maabara ya TEHAMA Bariadi kwa Gharama...

TEA Yajenga Maabara ya TEHAMA Bariadi kwa Gharama ya Sh Milioni 382

23 Oct, 2026
TEA Yajenga Maabara ya TEHAMA Bariadi kwa Gharama ya Sh Milioni 382

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, imeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini kwa kufadhili ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA katika shule za sekondari.

Shule ya Sekondari ya Bariadi, iliyopo mkoani Simiyu, ni miongoni mwa shule zilizonufaika na ufadhili huo, ambapo TEA imetumia jumla ya Shilingi milioni 382 kujenga maabara ya TEHAMA.

Maabara hiyo ina uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 90 kwa wakati mmoja, hatua inayotarajiwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, kuongeza fursa za wanafunzi kupata ujuzi wa kidijitali na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika elimu.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa TEA, CPA Richard Mazinge, amesema kuwa mradi umetekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakiwa.