Published at: Thu, Dec 7, 2023 4:36 PM
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu), Dkt. Franklin Jasson Rwezamula, leo tarehe 24 Mei, 2024 ametembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Jijini Dodoma kwa lengo la kupata taarifa za utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.
Katika ziara hiyo fupi ya kikazi, Dkt. Rwezamula amekutana na kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa TEA ambapo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa na Mfuko wa Kuendeleza ujuzi (SDF).
Aidha, ametumia fursa hiyo kukumbusha TEA kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa namna ambayo itaendana na maboresho ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambayo pamoja na mambo mengine imefanya mabadiliko ya mitaala ya elimu. “Lazima TEA ijihusishe katika kufanikisha mageuzi makubwa ya kielimu yanayoendelea hivi sasa.” Amesema