The United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA), YATOA UFADHILI WA MILIONI 300 KWA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA CHA MWALIMU JULIUS K. NYERERE

Published at: Thu, Dec 7, 2023 1:46 PM

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere Prof. Dominic Kambarage (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (kulia) wakikabidhiana hati za makubaliano ya ufadhili wa Shilingi Millioni 300 utakaotolewa na TEA kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi na kutengeneza mtaala katika Kampasi ya Butiama ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Julius K Nyerere kwenye hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Prof. Lesakit Mellay Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti.