The United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

Mbunge wa Tabora kaskazini Mhe. Almas Maige akiwa na Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Bw. Masozi Nyirenda kwenye Ofisi za TEA Ilazo - Dodoma alipofika kutoa shukrani kwa miradi ya elimu jimboni kwake

Published at: Thu, Nov 7, 2024 5:36 PM

Uboreshaji Miundombinu ya Elimu waleta Faraja Mkoani Tabora

Miradi ya uboreshaji Miundombinu ya Elimu Mkoani Tabora ambayo inatekelezwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, imekuwa faraja kubwa kwa wanafunzi na walimu ambao wamenufaika na miradi hiyo. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Tabora Kaskazini Mhe. Almas Maige alipotembelea ofisi za Mamlaka Jijini Dodoma Novemba 5, 2024 kwa lengo la kushukuru kwa miradi jimboni kwake lakini pia kuelezea hali halisi ya miundombinu ilivyo kwa baadhi ya shule.

Mhe. Maige akiwa ameongozana na Mbunge wa Igalula Mhe. Venant Daud pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Mohamed Mtulyakwaku wamekutana na kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Bw. Masozi Nyirenda kuhusu miradi mbalimbali ya uboreshaji miundombinu inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

Nyirenda amewashukuru viongozi hao kwa kutambua mchango wa TEA kwenye maeneo yao na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano hasa kwenye usimamizi wa miradi ili ikamilike kwa wakati na kuinua kiwango cha elimu bora kwa wote.