The United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

PROF. MKENDA AHIMIZA WANANCHI KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU

Published at: Tue, Sep 17, 2024 12:54 PM

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amehimiza watanzania kuona fahari ya kutoa kwa hiari michango ya kusaidia maendeleo ya elimu nchini hasa kwa kuchangia shule walizosoma ili kusaidia jitiihada za Serikali katika kuboresha Mazingira ya kujifunza na kufundishia.

 Prof. Mkenda ametoa wito huo alipokuwa akifungua na kukabidhi mradi wa nyumba za walimu katika Shule ya Msingi Msinune katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani zilizojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Flaviana Matata kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa kwa thamani ya Sh, milioni 150.

 

Waziri Mkenda amesema uamuzi wa Serikali wa kutoa Elimu bila ada kuanzia elimu ya awali hadi ya kidato cha sita katika shule za umma haizuii wananchi kutoa michango ya Elimu katika maeneo yao. “ Wananchi wamekuwa wepesi kutoa michango katika masuala ya kijamii ikiwa ni pamoja na harusi na misiba hivyo ari hiyo waielekeze kwenye sekta ya Elimu pia.”

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata amehimiza mtanzania mmoja mmoja kuchangia katika jitihada za kuboresha sekta ya elimu ambapo amesema nchi  itajengwa na watanzania wenyewe na sio kutegemea wafadhili kutoka nje

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu (TEA), Bahati Geuzye amesema Mamlaka imetumia Sh Bilioni 1.7 kufadhili miradi mbali mbali ya Elimu katika mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2020/2021