The United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

TAASISI ZA ELIMU ZAKUMBUSHWA KUSHIRIKISHA WAHITIMU KUKUSANYA RASLIMALI ZA KUBORESHA MIUNDOMBINU

Published at: Thu, Dec 7, 2023 3:59 PM

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bahati Geuzye ameshauri taasisi za elimu ikiwa ni pamoja na shule za msingi kuwashirikisha wahitimu wake (alumni) katika kukusanya na kuchangia  raslimali za kuboresha miundombinu ya elimu ya shule husika.

Mkurugenzi Mkuu wa TEA ametoa ushauri huo katika shule ya msingi Chamwino ya jijini Dodoma, tarehe 13 Oktoba, 2022 alipokuwa Mgeni Ramsi katika mahafali ya 19 ya wahitimu wa elimu ya msingi.

Amesema Shule ya Msingi Chamwino ambayo  imeanzishwa miaka ya 1950 itakuwa na wahitimu wengi wanaohudumu katika fani  mbali mbali, hivyo ni vyema shule ikawashirikisha katika jitihada za kukusanya raslimali za kuboresha miundombinu ya shule.

Akizungumza na wahitimu, Mkurugenzi Mkuu wa TEA amewakumbusha kila mmoja wao kudhamilia kwa dhati kupata elimu na maarifa zaidi.“Serikali imeweka mazingira mazuri zaidi kwa kutoa elimu bila malipo kuanzia ngazi ya  awali hadi  masomo ya kidato cha tano na sita,  hivyo,  kila mmoja wa wahitimu ana fursa nzuri ya kupata elimu” amesema.

Pia amesisitiza wahitimu kuzingatia  mafundisho na malezi bora kutoka kwa walimu, wazazi na walezi na kuepuke makundi yanayoweza kuwaingiza kwenye vitendo vya kihalifu na vitendo vinavyoenda kinyume na maadili na tamaduni za kitanzania

 

Awali katika risala yao wahitimu wameomba TEA kuboresha miundombinu  ya elimu  kwa kukarabati pamoja na kutoa ufadhili wa ujenzi wa  madarasa, matundu ya vyoo, ofisi za walimu, uzio wa shule pamoja na kuchimbiwa kisima cha maji ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TEA amesema watashirikiana na uongozi wa chuo katika kutafuta suluhu za changamoto hizo kwa kadri    

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma inayofanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. TEA inaratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao unasaidia jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa. Pia TEA inaratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia