Published at: Wed, Oct 1, 2025 9:15 AM
TEA NA UNICEF WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU NA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) inaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa vitendo katika shule za sekondari nchini.
Kwa sasa, TEA na UNICEF wanatekeleza mradi wa ukarabati wa maabara tatu za sayansi katika Shule ya Sekondari Masanga, iliyopo Manispaa ya Kigoma, mkoani Kigoma.
Mradi huu unagharimu takribani Shilingi milioni 64.6, na tayari umefikia hatua za mwisho za umaliziaji.
Lengo kuu la ukarabati huu ni kuhamasisha wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo, kuibua vipaji, maarifa na stadi za kazi miongoni mwao kwa maendeleo ya taifa letu.