The United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

TEA yaibuka kidedea maonesho ya Kitaifa ya Kazi za Utamaduni na Sanaa

Published at: Wed, Oct 1, 2025 11:33 AM

TEA YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA KITAIFA YA KAZI ZA UTAMADUNI NA SANAA

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma kwenye Maonesho ya Kwanza ya Mfuko wa Utamaduni yaliyofanyika kuanzia tarehe 24 – 30 Aprili 2025 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
TEA ilikuwa miongoni mwa taasisi zaidi ya 30 zilizoshiriki maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza shughuli za kitamaduni nchini.
Vigezo vilivyotumika katika utoaji wa tuzo vilihusisha:
•    Muonekano wa banda,
•    Utoaji wa huduma kwa wageni waliotembelea,
•    Ufanisi katika muda wa kutoa huduma (kufungua na kufunga).
Tuzo hiyo ilitolewa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Prof. Paramaganda Kabudi, ambaye alipongeza taasisi shiriki kwa mchango wao katika kuendeleza sekta ya utamaduni na sanaa nchini.
Ushindi huu unaonesha dhamira ya dhati ya TEA ya kuimarisha ushirikiano na wadau huku ikibaki mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo ya elimu na kukuza thamani za kitamaduni kwa jamii.