United Republic of Tanzania

Tanzania Education Authority

Managing The Education Fund

TEA YAPATA MWENYEKITI MPYA WA BODI

Published at: Tue, Aug 27, 2024 3:21 PM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia tarehe 15 Juni 2023.

Dkt. Akwilapo anachukuwa wadhifa huo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice Mbago kumaliza muda wake.

 Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kwa sasa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma inayofanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. TEA inaratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao jukumu lake kuu ni kutafufa rasilimali fedha na vifaa, kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ya sekta ya Elimu ndani na nje ya Tanzania ili kusaidia jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa