News

Wadau na wachangiaji wa Mfuko wa Elimu wa Taifa kukutana kwa siku moja katika Kongamano litakalofanyika katika Ukumbi wa Maktaba Mpya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 24 Juni 2021.
June 22, 2021
Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) inapenda kuwatangazia wananchi wote kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara wa vifaa chakavu vilivyopo katika ofisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo Mikocheni B Mtaa wa Bima mkabala na kituo kidogo cha polisi cha Mikocheni. Mnada huo utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 28 mwezi Juni, 2021 saa nne (4.00) asubuhi.
June 22, 2021
WADAU WA ELIMU WAHIMIZWA KUCHANGIA MFUKO WA ELIMU
April 01, 2021

1. Utangulizi

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mwaka 2017, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliipatia TEA jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazohusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi kwa lengo la kuzalisha ajira (ESPJ) unaotekelezwa na Wizara hiyo ukipata ufadhili toka Benki ya Dunia. Programu ya ESPJ ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Ujuzi (National Skills Development Strategy-NSDS: 2016-2021).

Maeneo muhimu yanayolengwa katika utekelezaji wa programu ya ESPJ ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji na pia kuongeza uwiano wa wataalam wa fani mbalimbali katika Sekta sita za kipaumbele (Kilimo na Kilimo Biashara, Utalii na huduma za Ukarimu, Nishati, Ujenzi, Uchukuzi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHEMA) zenye mchango mkubwa wa kiuchumi nchini.

Ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wenye mahitaji ya ujuzi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania imeanzisha Mpango wa Ufadhili (Bursary Scheme) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi. Mpango huu umelenga kuwezesha mafunzo ya ujuzi kwa vijana kutoka makundi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate uwezo wa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji zenye tija.

Tangazo la kukaribisha maombi ya ufadhili lilitangazwa mapema mwezi Septemba 2020 katika magazeti na tovuti ya TEA. Baada ya kupokea na kupitia maombi yaliyotumwa kuomba ufadhili, jumla ya wanufaika 2,102 wamekidhi vigezo vya kupatiwa Ufadhili wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi Kwa Makundi Maalumu na Vijana Wanaoishi Katika Mazingira Magumu. Orodha ya Wanufaika imeambatanishwa katika tangazo hili.

 

 

Orodha ya Majina ya wanufaika

January 29, 2021

NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHE. OMARY JUMA KIPANGA (MB) ATEMBELEA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA

January 11, 2021

UZINDUZI WA DURU YA PILI YA RUZUKU YA MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (SDF)

October 08, 2020
Utangulizi Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
September 18, 2020
Mkurugenzi Mkuu wa TEA ashiriki Uzinduzi wa Jengo la Utawala KIST, ambapo TEA Ilichangia Kiasi cha Sh.Milioni mia mbili (Sh 200,000,000). Mradi umefadhiliwa kwa ufadhili wa TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
May 27, 2020
EXTENSION OF THE DEADLINE FOR SUBMISSION OF SKILLS DEVELOPMENT FUND (SDF) PROPOSALS TO 25TH JULY 2019 AT 1:00 PM
July 23, 2019
Tanzania Education Authority (TEA) is hereby inviting your Institution to prepare and submit a comprehensive proposal for Skill Development Fund (SDF) Grant. The timeline for submission of the proposals is 21 days from 1st to 21st July 2019 through the SDF Skills Management Information System, which was used for submission of the Concept Notes.
July 02, 2019

Pages